Tuesday, May 16, 2017

NINGEKUWA BARCELONA AU BAYERN NINGETIMULIWA - GUARDIOLA.

MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema angeweza kutimuliwa na klabu za zamni alizopitia za Barcelona na Bayern Munich kama angemaliza msimu bila kutwaa taji. City wameshindwa kupata taji lolote katika msimu wa kwanza wa Guardiola huku wakiwa bado hawajapata uhakika wa kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza. City walitolewa katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, nusu fainali ya Kombe la FA na mzunguko wan ne wa Kombe la Ligi. Akizungumza na wanahabari, meneja huyo raia wa Hispania amesema kwa jinsi alivyomaliza msimu kama angekuwa katika klabu kubwa lazima angetimuliwa. Meneja huyo aliendelea kudai kuw akama ingekuwa Barcelona au Bayern lazima angetimuliwa kwasababu hakushinda chochote.

No comments:

Post a Comment