Tuesday, May 16, 2017

CAVANI ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA LIGUE 1.

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain-PSG, Edinson Cavani amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa Ligue 1 na wachezaji wake wa kulipwa jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay amefunga mabao 35 katika ligi msimu huu na PSG inaweza kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligue 1 nyuma ya vinara Monaco. Meneja wa Monaco Leonardo Jardim alitwaa tuzo ya kocha bora wa msimu huku tuzo ya mchezo bora anayechipukia ikienda kwa Kylian Mbappe, na Danijel Sibasic akiteuliwa kuwa kipa bora. Monaco wanaweza kutwaa taji lao la kwanza la Ligue 1 toka mwaka 200 kama wakiepuka kufungwa na St Etienne kesho. Kiungo wa Chelsea N’Golo Kante ameteuliw akuwa mchezaji bora wa Ufaransa anayecheza ligi ya nje.

No comments:

Post a Comment