Tuesday, May 16, 2017

REAL BETIS YAMFUKUZIA NOLITO.

KLABU ya Real Betis imeanza mazungumzo na Manchester City kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Nolito kwa kitita cha paundi milioni 3.4. Nolito mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na City kwa kitita cha paundi milioni 13.8 akitokea Celta Vigo Julai mwaka jana na kufanikiwa kucheza mechi 19 za Ligi Kuu chini ya Pep Guardiola na kufunga mabao manne. Hata hivyo, amefanikiwa kuanza katika mchezo mmoja pekee kwa Kombe la FA dhidi ya Huddersfield mwaka huu. Betis inayoshikilia nafasi ya 15 La Liga, itakuwa klabu ya nne ya Hispania kwa Nolito ingawa mashahara wake wa paundi 100,000 kwa wiki unaweza kuwa tatizo kwa timu hiyo. Guardiola amepanga kukisuka upya kikosi chake baada ya kumaliza msimu bila kupata taji lolote.

No comments:

Post a Comment