Tuesday, May 16, 2017

MTOTO WA BEBETO ASAJILIWA SPORTING LISBON.

MTOTO wa nguli wa zamani wa Brazil na mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 1994, Bebeto aitwaye Mattheus Oliveiro amejiunga na klabu ya Sporting Lisbon kwa mkataba wa miaka mitano. Kiungo huyo wa ushambuliaji mwenye umri wa miaka 22 ametua Sporting akitokea klabu ya Estoril ya Ureno baada ya kuanza soka lake jijini Rio de Janeiro kwenye timu ya Flamengo. Oliveiro alikuwa ndio kwanza ana siku kadhaa wakati baba yake ambaye jina lake kamili ni Jose Roberto Gama de Oliveira akiisaidia Brazil kutwaa taji la nne la Kombe la Dunia. Bebeto ambaye kwasasa ni Mbunge katika jimbo la Rio, alifunga mabao matatu katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Marekani. Baada ya kufunga bao dhidi ya Uholanzi katika mchezo war obo fainali uliofanyika Dallas, Bebeto alivuta hisia za mashabiki duniani kote pele alipokwenda kushangilia huku akionyesha ishara ya kubeba mtoto kwa ajili ya kijana wake huyo aliyezaliwa.

No comments:

Post a Comment