Tuesday, May 16, 2017

MOURINHO, GUARDIOLA KUKUTANA NA MAREKANI.

KLABU za Manchester United na Manchester City zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa kirafiki jijini Houston, Texas Julai mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza kwa Manchester Derby kuchezwa katika ardhi ya ugenini. Timu hizo zinatarajiwa kukwaana na Julai 20 katika Uwanja wa NRG Julai 20 ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Kombe la Ubingwa wa Kimataifa. Kiangazi mwaka jana timu zilitakiwa kukutana jijini Beijing, China lakini mchezo uliahirishwa kutokana na hali ya mbaya ya hewa iliyoharibu sehemu ya uwanja uliopaswa kutumika. Klabu zote zilithibitisha ushiriki wao katika mchezo huo huku ofisa mkuu wa City Ferran Soriano akidai kuwa utakuwa mchezo kipekee haswa kutokana na na kuchezwa nje ya Uingereza kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment