Wednesday, May 17, 2017

BEKI LA LEVERKUSEN LAIKACHA MAN CITY.

BEKI wa Bayer Leverkusen, Benjamin Henrichs amesaini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka Juni mwaka 2022. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, mkataab wake wa sasa ulikuwa unamalizika mwaka 2020 na Manchester City sambamba na Bayern Munich wote wanaaminika kumuwania kiungo huyo. Lakini Henrichs sasa amemaliza tetesi zote zilizozagaa kwa kuongeza mkataba wa miaka miwili na Leverkusen. Akizungumza na wanahabari beki huyo wa kulia amesema ni jambo kubwa kwa klabu hiyo ambayo amekuwa akiitumikia kwa kipindi cha miaka 13 kumpa nafasi nyingi. Henrichs aliendelea kudai kuwa anafurahi kwa kuwa mchezaji rasmi wa kulipwa katika klabu hiyo na hata kuitwa katika timu ya taifa ya Ujerumani.

No comments:

Post a Comment