Wednesday, May 17, 2017

MATAJIRI WA LEICESTER KUNUNUA TIMU UBELGIJI.

WAMILIKI wa Leicester City, King Power International wamekubali kuinunua klabu ya OH Leuven ya Ubelgiji. Klabu hiyo ya daraja la pili, inatoka mashariki mwa mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, na iliepuka kidogo kushuka daraja la tatu msimu huu. Bodi ya klabu hiyo iliweka muda wa kutafuta mwekezaji na kudai kuwa King Power ndio mzabuni pekee ambaye aliweka wazi mipango yake kwenye maombi yaliyotumwa. OH Leuven ilishuka kutoka Ligi Kuu ya Ubelgiji msimu wa 2015-2016 lakini wamedai kuwa mmiliki mpya atawawezesha kiuchumi ili kuhakikisha wanarejea Ligi Kuu haraka iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment