Wednesday, May 17, 2017

BENZEMA HAJAKATA TAMAA KUITWA UFARANSA.

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Karim Benzema bado hajakata tama na kurejea tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa pamoja na kuachwa na kocha Didier Deschamps kufuatia kashfa ya mkanda wa ngono miezi 18 iliyopita. Benzema alisimamishwa kuitumikia Ufaransa Desemba mwaka 2015 baada ya kushitakiwa kwa tuhuma za kuwa na ushirikiano na watu waliokuwa wakimsumbua mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena juu ya mkanda huo wa ngono. Octoba mwaka jana rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa-FFF, Noel Le Draet alidai kuwa ni ruksa kwa Deschamps kumuita kwenye kikosi chake Benzema kama aataona anamfaa. Benzema mwenye umri wa miaka 29 ambaye ahajaitwa toka Ufaransa ilipoifunga Armenia mabao 4-0 Octoba mwaka 2015, amesema bado hajapata ufafanuzi wowote kutoka kwa Deschamps wa kwanini anaendelea kumuacha kwenye kikosi chake.

No comments:

Post a Comment