Wednesday, May 17, 2017

GYAN KUENDELEA NA UNAHODHA BLACK STARS.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Ghana, Black Stars, Kwasi Appiah amemuacha nahodha wa kikosi hicho Asamoah Gyan kuendelea kushikilia nafasi yake hiyo. Kufuatia ujio wa Appiah mjadala mkubwa ulikuwa umezuka kuwa nani haswa kocha huyo atamchagua kama nahodha kwneye kikosi chake. Akizungumza na wanahabari, Appiah amesema hakuna lolote lililobadilika hivyo kumaanisha kuwa kutakuwa hakuna mabadiliko yeyote kwenye nafasi ya unahodha wa timu. Appiah alifafanua kuwa kama Gyan akiwa mgonjwa au majeruhi nahodha msaidizi Andre Ayew atashika nafasi hiyo na hivyo ndivyo imekuwa kwa miaka mingi sasa.

No comments:

Post a Comment