Wednesday, May 17, 2017

ARSENAL HAINA HAJA YA PICKFORD - WENGER.

MENEJA wa Arsenal, Arsee Wenger amesisitiza kipa wa Sunderland Jordan Pickford hayuko katika mipango yao kwani klabu hiyo ina watu wa kutosha kujaza nafasi hiyo. Pickford amekuwa kwenye kiwango cha juu pamoja na msimu mbovu wa Sunderland iliyoshuka daraja na kulikuwa na na taarifa kuwa Arsenal wamekuwa wakimuwania kipa huyo. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 alionyesha kiwango kikubwa kwa kuokoa michomo kadhaa katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata Arsenal jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu. Hata hivyo, Wenger amesema Pickford ambaye pia amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na Manchester City na Manchester United, atapata ushindani mkubwa sana Emirates. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Arsenal kwasasa hadhani kama inahitaji kipa kwani waliopo wanatosha kwa nafasi zao.

No comments:

Post a Comment