Thursday, May 18, 2017

DRAXLER AMTAKA OZIL KWENDA PSG.

KIUNGO wa kimataifa wa Ujerumani, Julian Draxler amedai kuwa kiungo wa Arsenal Mesut Ozil anapaswa kujiunga na Paris Saint-Germain-PSG. Ozil amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Arsenal, huku meneja Arsene Wenger akisubiri msimu umalizike ili waweze kujadili masuala ya mkataba ya mpya. Draxler ambaye amesema alikataa ofa ya kwenda Ligi Kuu ya Uingereza kwa ajili ya PSg Januari mwaka huu, amesema Ozil atafurahia maisha jijini Paris. Akizungumza na BBC, Draxler amesema angependa kucheza na Ozil kila siku kwani kwa upande wake ni mchezaji mkubwa. Draxler aliendelea kudai kuwa anafurahia anapokuwa naye mazoezi na kwenye mechi wakiwa katika majukumu ya kimataifa na Ujerumani.

No comments:

Post a Comment