Thursday, May 18, 2017

WANAOJIRUSHA SASA KUPATA ADHABU UINGEREZA.

WACHEZAJI soka ambao huwa wanapenda kujirusha nchini Uingereza wanaweza kukabiliwa na adhabu ya kufungiwa kuanzia msimu ujao. Chama cha Soka cha Uingereza-FA kinatarajia kupiga kura kuhusiana na suala hilo katika mkutano wake mkuu wa mwaka unaofanyika leo na kuna kila dalili kuwa ombi hilo litapitishwa. FA itahitahi kuungwa na Ligi Kuu, Ligi ya Soka la Uingereza na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa ili mabadiliko hayo yaweze kupita. Kama sheria hiyo ikipita, jopo maalumu la FA litakuwa likikaa kupitia mechi zilizochezwa mwishoni mwa wiki kuona kama kuna tukio kama hilo na kuchukulia hatua. Sheria hiyo itakuwa ikifanya kazi hata kama mwamuzi wa mchezo hakuona tukio na kuliandika kwenye taarifa yake.

No comments:

Post a Comment