Thursday, June 29, 2017

ARTURO VIDAL AELEZA ALICHOWAAMBIA BRAVO KABLA YA KUOKOA PENATI TATU.

KIUNGO wa kikosi cha timu ya taifa ya Chile, Arturo Vidal amebainisha alichosema kipa Claudio Bravo kwa wachezaji wenzake kabla ya kuokoa penati tatu za Ureno katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho jana. Mchezo huo ulikwenda katika dakika za nyongeza kufuatia sare ya bila kufungana katika Uwanja wa Kazan Arena kabla ya kufikia hatua ya changamoto ya mikwaju ya penati ambayo iliivusha Chile katika hatua ya fainali. Ureno mabingwa wa Ulaya walijikuta wakipewa wakati mgumu kufuatia Bravo kupangua penati tatu za Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na Nani. Akizungumza na wanahabari, Vidal amesema Bravo aliwaambia kabla ya penati kuwa ataokoa mbili au tatu na alifanya hivyo. Mara baada ya mchezo huo, Bravo alilalamika kuwa alikuwa ameumia lakini aliamua kuendelea ili kuisaidia timu yake kusonga mbele. Mabingwa hao wa Amerika Kusini sasa watakutana na aidha Ujerumani au Mexico katika hatua ya fainali itakayofanyika huko Krakow.

No comments:

Post a Comment