Thursday, June 29, 2017

BARCELONA KUCHEZA NA CHAPECOENSE.

KLABU ya Barcelona inatarajiwa kuwa wenyeji wa Chapecoense katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Agosti 7 mwaka huu ili kutoa mchango wao kwa wale waliofariki dunia wakati ndege iliyokuwa imeibeba timu hiyo ya Brazil ilipoanguka Novemba mwaka jana. Wachezaji watatu pekee ndio waliosalimika katika ajali hiyo Novemba 29, wakati watu 71 kati ya 77 waliokuwepo ndani yake walifariki. Barcelona wamesema wanatarajia mchezo huo utaisaidia Chapecoense kujijenga kama taasisi na kurejea katika ushindani kama ilivyokuwa kabla ya ajali. Mshindi kwenye mchezo huo utakaofanyika katika Uwanja wa camp Nou anatarajiwa kupewa taji la Joan Gamper. Ajali hiyo ilitokea wakati Chapecoense wakisafiri kwenda kupambana na Atletico Nacional ya Colombia katika faiali ya Copa Sudamericana. Mabeki Neto na Alan Ruschel na kipa Jacson Follmann ambaye alikatwa mguu ndio miongoni mwa watu sita waliosalimika, wakati wachezaji 19 na benchi lote la ufundi walipoteza maisha.

No comments:

Post a Comment