Thursday, June 29, 2017

RONALDO ATHIBITISHA KUPATA WATOTO WENGINE WAWILI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amethibitisha kuwa amekuwa baba tena wa watoto wawili wa kiume waliozaliwa wakati wa michuano ya Kombe la Shirikisho inayoendelea huko nchini Urusi. Ureno ilienguliwa katika michuano hiyo jana kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-0 na Chile kufuatia timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida na ule wa nyongeza. Ronaldo alionyesha kusikitishwa kwa kutolewa huko na kuthibitisha taarifa za kuzaliwa kwa watoto wake hao ambazo zinaweza kumfanya kukosa mchezo wa mtoano kutafuta mshindi wa tatu Jumapili hii. Ronaldo alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook akida alikuwa amejitoa kwa kila kitu kuisaidia nchi yake katika michuano hiyo pamoja na kuwa watoto wake walikuwa wamezaliwa. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa amesikitishwa kwa kushindwa kufikia malengo waliyokuwa wamejiwekea lakini ana matumaini wataendelea kuwapa furahi mashabiki wa soka wa Ureno.

No comments:

Post a Comment