RAIS wa Bayern Munich, Uli Hoeness ameonyesha kuondoa uwezekano wa kumsajili nyota wa Arsenal Alexis Sanchez kwa kudai kuwa kikosi chao kinapaswa kujengwa na wachezaji vijana zaidi kuliko wale wazoefu. Mabingwa hao wa Bundesliga wamekuwa wakihusishwa kwa kiasi kikubwa na tetesi za kumuwania nyota huyo wa kimataifa wa Chile katika miezi ya karibuni, ingawa hivi sasa Manchester City ndio wanaoonekana kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na mipango ya Bayern, Hoeness amesema kikubwa wanachofanya ni kujenga kikosi chao kupitia wachezaji vijana. Hoeness aliongeza kuwa kamwe hawawezi kujenga kikosi bora cha baadae kwa kununua mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 29 au 30 kwa kiasi cha euro milioni 100, hizo sio sera zao.
No comments:
Post a Comment