Tuesday, June 20, 2017

CONTE KUSAINI MKATABA MPYA BAADA YA CHELSEA KUKUBALI KUTOA FUNGU LA USAJILI.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa paundi milioni 9.5 ili kuendelea kubaki katika klabu hiyo mpaka mwaka 2021 baada ya kuhakikishiwa kuwa atapewa fungu la kusajili kufuatia kutoelewana wiki iliyopita. Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia ameonekana kumaliza tofautia na Conte Jumapili iliyopita kufuatia kudokeza suala la usajili na mkataba mpya wa meneja huyo. Conte anatarajiwa kuwa meneja wa saba anayelipwa zaidi duniani na watu kwa nchini Uingereza kama akitia saini mkataba huo mpya. Hivi karibuni kulikuwa kumezuka tetesi za mustakabali wa Conte kufuatia Muitaliano huyo kuweka wazi kutofurahishwa na jinsi suala la usajili lilivyo katika klabu hiyo. Conte anatarajiwa kurejea kutoka likizo Julai 7 mwaka huu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya kabla ya Chelsea haijakutana na Arsenal katika mchezo wa Ngao ya Hisani.

No comments:

Post a Comment