Tuesday, June 20, 2017

BAADA YA RONALDO, MOURINHO NAYE ATUHUMIWA KUKWEPA KODI.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho anatuhumiwa kwa makosa ya kukwepa kodi kufuatia uchunguzi wa waendesha mashitaka wa Hispania wakati akiifundisha Real Madrid. Mourinho raia wa Ureno anatuhumiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia paundi milioni 2.9 kati ya mwaka 2011 na 2012 ambapo bado hajatoa kauli yeyote kuhusiana na tuhuma hizo. Waendesha mashitaka wamedai kuwa hakuweka wazi mapato yake kwa ajili ya haki ya matumizi ya picha zake. Hivi karibuni majina kadhaa makubwa katika soka yamekuwa yakituhumiwa kukwepa kodi nchini Hispania. Miongoni mwa majina hayo ni nyota wa Madrid Cristiano Ronaldo ambaye anatarajiwa kufikishwa kizimbani kutoa utetezi wake Julai 31 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment