Tuesday, June 20, 2017

OZIL AONYESHA DALILI ZA KUBAKI ARSENAL.

KIUNGO wa Arsenal, Mesut Ozil amedokeza kubaki Emirates kwa kuzungumzia ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya huko Australia. Mustakabali wa nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani bado haujakaa sawa kufuatia mkataba wake kutarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao. Bado hajakubali kusaini mkataba mpya lakini Ozil alweka pembani suala la yeye kuondoka na kuzungumzia jinsi alivyokuwa na hamu kubwa ya kusafiri na timu hiyo katika ziara la maandalizi ya msimu ujao. Akizungumza na wanahabari, Ozil amesema amesikia Sydney ni mji mzuri na kuna watu wengi wazuri wanaishi kule. Ozil aliendelea kudai kuwa hafahamu sana kuhusu Australia lakini ziara hiyo itakuwa nafasi nzuri ya kuona mji, watu na anafurahia kwenda huko na Arsenal.

No comments:

Post a Comment