Tuesday, June 20, 2017

RAIS WA MADRID KUTETA NA RONALDO.

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amesema hajazungumza na Cristiano Ronaldo kuhusu mustakabali wake lakini anatarajia kufanya hivyo baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Shirikisho. Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 anadaiwa kutaka kuondoka Hispania baada ya kutuhumiwa na makosa ya ukwepaji kodi. Mshambuliaji huyo ambaye yuko nchini Urusi na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, alisaini mkataba mpya wa miaka mitano Novemba mwaka jana lakini amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea Manchester United. Perez ambaye alichaguliwa tena kuiongoza klabu hiyo jana, amesema jambo pekee analoweza kusema ni kuwa Ronaldo ni mchezaji wa Madrid. Perez aliendelea kudai kuwa kwasasa hataki kuisumbua timu ya Ureno kwakuwa wako katika michuano muhimu hivyo atasubiri mpaka itakapomalizika.

No comments:

Post a Comment