Saturday, March 2, 2013
NADAL KUVAANA NA FERRER FAINALI YA MICHUANO YA WAZI YA MEXICO.
MCHEZAJI tenisi nyota Rafael Nadal amefanikiwa kumfunga Mhispania mwenzake Nicolas Almagro na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano wazi ya Mexico. Nadal ambaye amerejea karibuni baada ya kukaa nje kwa kipindi cha miezi saba akijiuguza anatarajiwa kukutana na bingwa mtetezi wa michuano hiyo David Ferrer ambaye naye pia ni raia wa Hispania. Toka arejee uwanjani nyota huyo ambaye amewahi kunyakuwa mataji 11 ya Grand Slam amekuwa mshindi wa pili katika michuano ya wazi ya Chile kabla ya kuja kushinda michuano ya wazi ya Brazil wiki mbili zilizopita. Nadal atakuwa akifukuzia taji lake la 38 dhidi ya Ferrer ambaye ameshinda mechi 19 mfululizo huku akifukuzia taji lake la tatu msimu huu.
BLATTER KUANZISHA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA UBAGUZI.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amesema wanatarajia kuanzisha kikosi kazi kwa ajili kupambana tatizo la ubaguzi wa rangi katika soka. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Edinburgh kabla ya mkutano wa bodi unaotarajiwa kufanyika baadae leo, Blatter amesema kikosi kazi hicho kitaongozwa na rais wa Shirikisho la Soka kwa nchi za Amerika kaskazini na kati na Caribbean-Concacaf Jeffrey Webb. Kwa muda mrefu mchezo wa soka umekuwa ukitawaliwa na matukio ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki hususani sehemu za Ulaya mashariki pamoja na adhabu mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa. Blatter amekiri kuwa ubaguzi ni tatizo kubwa katika mchezo wa soka ndio maana ameamua kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili kuangalia uwezekano wa kutokomeza mambo ya kibaguzi. Blatter pia atakutana na kiungo wa AC Milan Kevin-Prince Boateng baadae mwezi huu kujadili njia za kutumia kutokomeza ubaguzi baada ya mchezaji huyo kutengeneza vichwa vya habari kwa kuongoza wachezaji wenzake kutoka uwanjani baada ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi.
Friday, March 1, 2013
SINA MPANGO WOWOTE MAALUMU NA BALE - WENGER.
KLABU ya Arsenal imedai kuwa haina mpango wa kumuwekea ulinzi maalumu mshambuliaji nyota wa Tottenham Hotspurs Gareth Bale katika mchezo utakaozikutanisha timu hizo kesho. Tottenham inaweza kufifisha ndogo za Arsenal kukata tiketi kwa ajili ya kucheza michuano ya klabu bingwa ya Ulaya msimu ujao kama wakifanikiwa kuwafunga huku Bale akiwa kikwazo kikubwa kutoka kiwango cha juu alichokionyesha katika michezo yake ya hivi karibuni. Lakini meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye atamkosa beki wake wa kulia Bacary Sagna katika mchezo huo amesema hana mpango wa kumuwekea ulinzi mchezaji huyo kwani amepanga kuandaa kikosi chake kucheza kitimu ili kuhakikisha anaondoka na matokeo mazuri. Wenger amesema wachezaji wote wa Tottenham wana viwango tofauti hivyo itakuwa ni makosa kujiandaa kwa ajili kumzuia mchezaji mmoja kwani hatakuwa peke yake uwanjani. Kocha huyo aliendelea kusema amewaandaa vyema vijana wake kwa ajili ya mchezo huo ambao utazikutanisha timu hizo ambazo zote zinatoka kaskazini mwa jiji la London.
GFA LAWAANGUKIA WATOTO PELE.
SHIRIKISHO la Soka nchini Ghana-GFA limewaangukia watoto wa nguli wa zamani wa soka wa nchi hiyo Abeid Ayew Pele likiwaomba kuangalia upya uamuzi wao wa kujitoa kwa muda kuchezea timu ya taifa. GFA iliwaandikia barua rasmi Andres na mdogo wake Jordan Ayew wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa ikiwaomba kubadilisha uamuzi huo na kujaribu kutatua matatizo waliyonayo kwa mazungumzo. Andres aliandika barua kwenda shirikisho hilo kulitaka kumuondoa katika kipango kwani ameamua kupumzika kwa muda kwasababu ya kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya viongozi huku mdogo wake akidai shirikisho hilo halithamini mchango wake katika timu ya taifa ya nchi hiyo. Wadau mbalimbali wa michezo nchini Ghana akiwemo rais wa zamani wa GFA Dr Nyaho Tamakloe walilitaka shirikisho hilo kukaa na vijana hao kuangalia jinsi ya kutatua tatizo hilo kwa manufaa ya soka la nchi hiyo.
GIGGS AKUBALI KUONGEZA MKATABA UNITED.
WINGA machachari wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo. Mkataba huo mpya aliosaini Giggs mwenye umri wa miaka 23 utamuwezesha kuitumikia klabu hiyo yenye mashakani yake Old Traford mpaka Juni 2014 na kukamilisha misimu 23 akiwa mchezajiw a kikosi cha kwanza. Nahodha huyo wa zamani wa Wales alianza kucheza katika kikosi cha kwanza cha United Machi 2 1991 na amefunga mabao 168 katika mechi 931 alizocheza. Akihojiwa mara baada ya kuaini mkataba huo Giggs amesema anajisikia vyema na anafurahia soka lake zaidi kuliko ilivyokuwa kipindi cha nyuma. Naye meneja wa United Sir Alex Ferguson alimuelezea nyota huyo kama mchezaji mahiri ambaye anafaa kuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji wengine chipukizi wa klabu hiyo.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
FIFA YAWASILISHA MAREKEBISHO 10 YA KATIBA KWA WARAKA
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetuma mapendekezo 10 ya marekebisho ya Katiba yake kwa wanachama wake kwa njia ya waraka. Mapendekezo hayo yametumwa kwa kila nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320, ambapo wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho yao ya mabara watapiga kura ya ndiyo au hapa. Kwa upande wa Afrika, wanachama wa FIFA wanatakiwa kuwasilisha kura zao kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Baadhi ya mapendekezo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa FIFA (FIFA Congress). Makamu wa Rais wa FIFA na wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi wathibitishwe na FIFA Congress. Muundo wa Kamati ya Utendaji; nafasi moja ya vyama vya mpira wa miguu vya Uingereza (British FAs) sasa inahamishiwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA). Pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya FIFA anatakiwa kushiriki vikao vya Kamati ya Utendaji bila kuwa na haki ya kupiga kura. Uchaguzi wa Rais; mgombea anatakiwa kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama wanachama kutoka katika mabara mawili tofauti. Ukomo wa uongozi; kuanzisha vipindi vya uongozi. Ukomo wa umri; ukomo wa umri usiozidi miaka 72 wakati wa kugombea utekelezwe. Uwakilishi wa kutosha kwa makundi yenye maslahi katika FIFA; makundi yenye maslahi katika mpira wa miguu kama wachezaji wapate uwakilishi katika Kamati ya Mpira wa Miguu. Uteuzi wa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi sasa ufanywe na Mkutano Mkuu wa TFF.
WATAZAMAJI 13,398 WAZISHUHUDIA YANGA, KAGERA
Watazamaji 13,398 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Kagera Sugar lililochezwa juzi (Februari 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 77,117,000. Mechi hiyo namba 130 iliyochezeshwa na Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 42 kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 45 na Haruna Niyonzima. Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 18,291,297.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,763,610.17. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 11,908 na kuingiza sh. 59,540,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 80 na kuingiza sh. 1,600,000. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,300,659.97, tiketi sh. 3,348,990, gharama za mechi sh. 5,580,395.98, Kamati ya Ligi sh. 5,580,395.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,790,197.99 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,170,153.99.
POLISI KUIKABILI OLJORO KUNG’ANG’ANIA VPL
Polisi Morogoro inaikaribisha Oljoro JKT ya Arusha kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika mechi pekee ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itakayochezwa kesho (Machi 2 mwaka huu). Hata hivyo, timu hizo haziko katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa ambapo Yanga ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42 wakati Oljoro JKT inayofunzwa na Alex Mwamgaya ikiwa nazo 21 na Polisi Morogoro pointi 15.
Oljoro JKT iko katika nafasi ya tisa. Polisi Morogoro ambayo katika mzunguko wa pili imebadilika ikiwa chini ya Kocha Adolf Rishard inashika nafasi ya 12 ikiziacha mkiani Toto Africans yenye pointi 14 na African Lyon ambayo ina pointi 13. Ligi hiyo itaendelea Jumatano (Machi 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Oljoro JKT vs Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), African Lyon vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Chamazi) na Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar (Mkwakwani) wakati Machi 7 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Kagera Sugar (Azam Complex, Chamazi). Machi 9 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Yanga vs Toto Africans 9Uwanja wa Taifa), na Azam vs Polisi Morogoro (Azam Complex, Chamazi).
VILLA SQUAD KUIVAA ASHANTI UNITED FDL
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea kesho (Machi 2 mwaka huu) katika makundi yote matatu. Villa Squad itaivaa Ashanti United kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B. Kundi A ni mechi kati ya Kurugenzi ya Mafinga dhidi ya Mbeya City wakati Polisi Iringa vs JKT Mlale, na Majimaji vs Mkamba Rangers zilizokuwa zicheze kesho (Machi 2 mwaka huu), sasa zitaumana Machi 3 mwaka huu mjini Iringa na mjini Songea. Pia kundi B kesho (Machi 2 mwaka huu) ni Green Warriors vs Transit Camp (Mlandizi) wakati keshokutwa (Machi 3 mwaka huu) Polisi Dar vs Tessema (Karume) na Ndanda vs Moro United katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Mechi za kundi C kesho ni JKT Kanembwa vs Polisi Tabora (Lake Tanganyika), Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Karume, Musoma), Morani vs Pamba (Kiteto) na Mwadui vs Rhino Rangers (Kambarage, Shinyanga).

KAMPUNI YA TANZANIA MWANDI YAANZISHA MICHUANO YA AFRICAN YOUTH FOOTBALL TOURNAMENT
Kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kutambua kuwa Tanzania na Afrika nzima kuna vijana wengi ambao wana vipaji vya mpira wa miguu na hivyo wanachohitaji ni kuonyeshwa tu jinsi ya kuufikia ‘Ulimwengu Halisi’ wa Mpira duniani Tanzania Mwandi imeamua kuanzisha michuano ya African Youth Football Tournament ambayo itawashirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 21. Michuano hiyo itaambatana na mafunzo kwa siku tano ambapo vijana hao watapata mafunzo ya mpira wa Miguu (elimu, ujuzi na hata mbinu za uwanjani) kutoka kwa makocha wawili wa hapa nchini na watatu wa kimataifa kutoka nje ya nchi, kuanzia tarehe 10/06/2013 hadi tarehe 14/06/2013 katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Aidha, mafunzo yatafanyika nyakati za asubuhi na jioni wachezaji hao watashiriki Mashindano ya kucheza wao kwa wao ili kupata vijana 11 bora miongoni mwa wachezaji watakaoshiriki. Wachezaji Bora 11 watakaopatikana watakuwa mabalozi wa Mdhamini Mkuu wa Michuano ya African Youth Football Tournament na watapata fursa ya kutangazwa zaidi kimataifa na kutafutiwa vilabu vya kucheza soka Barani Ulaya katika nchi nane (Ufaransa, Ureno, Uswis, Ubelgiji, Uholanzi, Norway, Sweden na Denmark pamoja na barani Afrika na Asia. Ili kupanua wigo wa kuwatangaza kimataifa wachezaji wengi zaidi, Michuano hii pia itaalika skauti na mawakala wa soka wa kimataifa ili kufuatilia uwezo wa wachezaji hao asubuhi katika mazoezi na jioni kwenye michuano, kuwapata vijana bora ambao watapendelea kuwatafutia timu nje ya nchi kukipiga huko kwa makubaliano ambayo pande hizo mbili (mchezaji na wakala) zitaafikiana.
Miongoni mwa Mawakala ambao watakuwepo ni wakala wa Kimataifa wa Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro, Phillip Mwakikosa (Sweden) na wengine wengi. Hata hivyo kutokana na gharama kubwa za uandaaji wa Michuano hii, na ndio kwanza ikiwa inaanzishwa, Kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kujali mahitaji ya Kitanzania tumeweka kiingilio kwa mchezaji wa Tanzania kuwa shilingi laki tatu (Tsh. 300, 000) na mchezaji wa nje ya Tanzania Dola 500 za Kimarekani (USD 500). Fedha hizo zitagharamia malazi, chakula na mahitaji mengine yote kwa mchezaji pindi atakapokuwa kambini. Hii ni fursa adimu kwa vijana wa Kitanzania kuonyesha uwezo wao ili kutimiza ndoto za kucheza soka barani Ulaya, Asia na barani Afrika katika vilabu vikubwa huku ikikumbukwa kuwa mnamo Mwaka 2012 ni wachezaji wachache sana wa Kitanzania waliopata fursa ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kutokana na uchache wa mawakala na gharama hivyo kuletwa mawakala hao nyumbani Tanzania ni fursa pekee ya kufikia malengo. Mpaka sasa tayari Kampuni ina majina takribani ya vijana 10 wa Nje ya nchi (Uganda, Nigeria na Ghana) ambao wameomba kushiriki hivyo tunatoa wito kwa Watanzania kutoipoteza fursa ya kuletewa njia ya kuelekea kusakata soka Barani Ulaya mlangoni mwao. Lakini tunafahamu hali halisi ya maisha yetu kwahiyo nitoe wito kwa Wadhamini mbalimbali ambao tumewaomba kutusaidia kufanikisha Mashindano haya ambayo naamini yatalitangaza taifa letu na kulitangaza zaidi soka letu kimataifa. Pia udhamini wao utatuwezesha kupunguza hizi gharama kwa washiriki kutoka Tanzania na hivyo kuwachukua vijana wengi zaidi. Kampuni ya Tanzania Mwandi ni Kampuni binafsi ambayo imejikita katika kuendeleza sekta za utalii, michezo na burudani ndani na nje ya nchi na hivyo kuiongezea kipato nchi moja kwa moja ama kupitia kuwawezesha wananchi kama vile kuwatengenezea fursa za ajira vijana kupitia michezo. Fomu za ushiriki Michuano hii zinapatikana kupitia www.tanzaniamwandi.co.tz

Subscribe to:
Posts (Atom)