
Wednesday, March 5, 2014
JOHNSON AMPAKA MOURINHO.
RAUL ANAWEZA KUWA KOCHA WA MADRID - VALDANO.
MKURUGENZI wa zamani wa klabu ya Real Madrid Jorge Valdano anaamini kuwa Raul anaweza kurejea Santiago Bernabeu kama kocha mkuu katika siku zijazo na kujitengenezea jina kama ilivyo kwa Pep Guardiola. Raul aliondoka Madrid na kuhamia Schalke mwaka 2010 kabla ya kuondoka katika timu hiyo ya Ujerumani na kwenda Al Sadd miaka miwili baadae lakini Valdano hana shaka kwamba mshambuliaji huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 36 anaweza kurejea kuingoza klabu hiyo kwa mafanikio kama iliyokuwa alipokuwa mchezaji. Valdano amesema hana shaka kwamba hivi Raul anajipima kama anaweza kurejea Madrid akiwa kocha kwani anaweza kuongeza kitu muhimu kwa timu hiyo. Guardiola ambaye amewahi kucheza Barcelona alirejea tena katika timu hiyo akiwa kocha kati ya mwaka 2008 na 2012 akishinda mataji 14 kabla ya kuamua kupumzika kwa muda wa mwaka mmoja na kurejea kuinoa Bayern Munich.
MESSI HAHITAJI KOMBE LA DUNIA ILI AWEZE KUWA MCHEZAJI BORA - MARADONA.
NGULI wa soka nchini Argentina, Diego Maradona amesema nyota wa Barcelona Lionel Messi hahitaji kushinda medali ya Kombe la Dunia ili aweze kuhesabiwa kama mmoja wa wachezaji bora kuwai kutokea. Maradona aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichonyakuwa Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka 1986 amedai nyota huyo haitaji Kombe la Dunia ili kuwa mchezaji bora duniani. Maradona amesema kama akishinda Kombe la Dunia litakuw ajambo zuri kwa Argentina na kwake mwenyewe lakini hata akilikosa haiwezi kuondoa ubora wake kutokana na mafanikio aliyopata. Argentina ambao wameshinda taji la Kombe la Dunia mara mbili wanatarajiwa kucheza na Romania mechi ya kirafiki itakayochezwa jijini Bucharest baadae leo.
SIOGOPI KUACHWA KOMBE LA DUNIA - PODOLSKI.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ujerumani, Lukas Podolski amesisitiza kuwa haogopi kuachwa katika kikosi cha nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia lakini ana uhakika atachaguliwa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata majeruhi ya kuchanika msuli mwishoni mwa Agosti mwaka jana hatua ambayo ilipelekea kumuweka nje mpaka mwishoni mwa jana huku akifanikiwa kuanza katika mechi tano pekee katika klabu yake ya Arsenal msimu huu. Wakati ikiwa imebaki miezi mitatu kabla ya kuanza michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil, Podolski anajua anahitaji muda zaidi ili kuonyesha kuwa anastahili nafasi katika kikosi hicho kinachonolewa na Joachim Low lakini nyota huyo amesema ana uhakika na nafasi yake. Akihojiwa kabla ta mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Chile baadae leo Podolski amesema hana hofu juu ya nafasi yake katika kikosi cha Ujerumani kwasababu ana uzoefu wa muda mrefu kwa kucheza mechi na mashindano mengi. Podolski amesema baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu hivi sasa yuko fiti na tayari ameshazungumza na makocha wote wawili wa klabu na timu yake ya taifa. Ujerumani imepangwa kundi moja na timu za Ureno, Ghana na Marekani katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 12.
PIQUE AMUITA PUYOL MALAIKA ALIYETUMA KUWALINDA.
BEKI wa klabu ya Barcelona Gerard Pique amesema Carles Puyol amekuwa kama malaika mlinzi katika timu hiyo na amesikitishwa na taarifa kuwa ataondoka Camp Nou mwishoni mwa msimu. Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 amekuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kwa kipindi cha zaidi ya muongo mmoja lakini jana alitangaza nia yake ya kuondoka kwa mabingwa hao wa La Liga mwishoni mwa msimu huu ambapo mkataba wake unamalizika. Pique ambaye alirejea Barcelona akitokea Manchester United mwaka 2008 aliandika barua ya wazi katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook akielezea kuguswa na taarifa hizo za kuondoka kwa Puyol. Nyota huyo amesema anajua wakati umefika wa Puyol kuondoka lakini ngumu kukitizama kikosi cha Barcelona bila muongozo wa mkongwe huyo. Pique amesema atamkumbuka Puyol kwa mengi hususani mazungumzo yao katika vyumba vya kubadilishia nguo, ushauri na umahiri wake pindi awapo uwanjani.
ABIDAL ALAZWA TENA KWA SIKU MBILI.
KLABU ya Monaco imedai kuwa beki wake Eric Abidal alilazwa kwa muda wa siku mbili hospitalini kufuatia kupata maambukizi ya virusi. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitumia muda wa saa 48 akifanyiwa vipimo katika hospitali ya Princess Grace iliyopo Monaco kama sehemu ya tahadhari kutokana na maradhi ya saratani yaliyowahi kumpata kipindi cha nyuma. Abidal mwenye umri wa miaka 34 aligundulika kuwa saratani ya ini mwaka 2011 na kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine mwaka uliofuatia ili kutibu tatizo lake hilo. Hata hivyo taarifa ya klabu hiyo iliendelea kudai kuwa beki huyo aliruhusiwa na atafanya mazoezi na wenzake kama kawaida.
Tuesday, March 4, 2014
BENDTNER ACHOSHWA NA BENCHI ARSENAL.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Arsenal, Nicklas Bendtner amekiri kuwa hana furaha kwa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Denmark ameanza mara moja pekee katika kikosi cha kwanza msimu huu na kocha Arsene Wenger hivi karibuni amekuwa akimchezesha Yaya Sanogo katika mechi muhimu za Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya kama akikosekana Olivier Giroud. Akizungumza katika kambi ya timu yake ya taifa kabla ya mchezo dhidi ya Uingereza utakaochezwa katika Uwanja wa Wembley kesho, Bendtner amesema yuko fiti kwa ajili ya kucheza na kama utamkuta mchezaji anapenda kusugua benchi anadhani ni bora atafute kazi nyingine. Bendtner amesema anataka kucheza na yuko tayari kwasababu anafanya mazoezi vizuri suala la kutochaguliwa na kocha sio juu yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)