KLABU ya Swansea City imemtimua meneja wake Francesco Guidolin na nafasi kuchukuliwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley. Swansea hawajashinda mechi yeyote ya Ligi Kuu toka kuanza kwa msimu na sasa wanashika nafasi ya 17 katika msimamo. Bradley ambaye pia amewahi kuzifundisha Misri na klabu ya Stabaek ya Norway, anaiacha timu ya Le Havre inayoshiriki ligi daraja la pili Ufaransa na kwenda kuchukua nafasi ya Guidolin aliyeteuliwa Januari mwaka huu. Viongozi wa klabu hiyo wanadaiwa kuzungumza na makocha kadhaa kwa ajili ya nafasi hiyo akiwemo nahodha wa zamani wa kimataifa wa Wales Ryan Giggs. Kibarua cha kwanza cha Bradley mwenye umri wa miaka 58, kitakuwa kusimamia mchezo dhidi ya Arsenal Octoba 15 mwaka huu baada ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa kumalizika.
Monday, October 3, 2016
KIPA WA BARCELONA AOMBA RADHI KWA MADUDU ALIYOFANYA.
KIPA wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen amewaomba radhi wachezaji wenzake baada ya makosa yake aliyofanya kuisaidia Celta Vigo kupata ushindi wa mabao 4-3 na kuizuia timu hiyo kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga. Mabingwa hao wa Hispania ambao msimu uliopita pia walitandikwa na Celta Vigo, walijikuta wako nyuma kwa mabao matatu katika kipindi cha kwanza huku makosa ya Ter Stegen yakiwasaidia wenyeji kupata bao la kuongoza kupitia kwa Pione Sisto. Bao la kichwa la Gerard Pique na penati iliyofungwa na Neymar ilitoa matumaini kwa Barcelona katika kipindi cha pili lakini bao la kichwa la Pablo Hernandez lililotokana tena na makosa ya Ter Stegen yaliirudisha nyuma timu hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, kipa huyo wa kimataifa wa Ujerumani amesema walipambana mpaka mwisho lakini kuna baadhi ya makosa yaliyogharimu yalikuwa yak wake hivyo anaomba radhi kwa wachezaji wenzaji wenzake. Barcelona kwasasa waashikilia nafasi ya nne katika msimamo wa La Liga wakiwa alama mbili nyuma ya vinara Atletico Madrid.
SONG APATWA NA KIHARUSI.
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Rigobert Song amelazwa hospitali baada ya kuripotiwa kupatwa na maradhi ya kiharusi. Mmoja wa wanafamilia amedai kuwa nguli huyo mwenye umri wa miaka 40 alifikishwa hospitali jijini Younde akiwa hajitambui baada ya kushambuliwa na maradhi hayo. Song ameichezea mechi 137 nchi yake huku pia akiwahi kucheza katika klabu za Liverpool na West Ham United zinazoshiriki Ligi Kuu Uingereza. Nguli huyo amekuwa akifanya kazi kama kocha wa timu ya taifa ya Chad toka alipoteuliwa Octoba mwaka jana. Mchezaji mwenzake wa zamani wa Cameroon Samuel Eto’o sambamba na wachezaji wenzake wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher, Stan Collymore na Robbie Fowler wote walituma ujumba katika mitandao yao wa kijamii ya Twitter wakimpa pole nguli huyo.
DI MATTEO AONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA ASTON VILLA.
KLABU ya Aston Villa imemtimua meneja wake Roberto di Matteo baada ya kudumu katika kazi hiyo kwa siku 124 pekee. Villa kwasasa wanatafuta meneja mpya ambaye atakuwa wa nne katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kumtimua Muitaliano huyo ambaye ameshinda mechi moja kati ya 11 za ligi ya ubingwa alizosimamia. Di Matteo mwenye umri wa miaka 46 ambaye pia amewahi kuinoa Chelsea, aliteuliwa muda mfupi baada ya mfanyabiashara Dr Tony Xia wa China kuinunua klabu hiyo Juni 2. Msaidizi wa Di Matteo, Steve Clarke ndio amepewa mikoba ya muda kuiongoza klabu hiyo.
MOURINHO AKIFAGILIA KIKOSI CHAKE PAMOJA NA SARE.
MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amesisitiza kuwa kikosi chake kilicheza mchezo bora kwa msimu huu na wangeweza kufunga hata mabao saba dhidi ya Stoke City. Kauli hiyo ya Mourinho imekuja kufuatia sare ya bao 1-1 waliyopata katika Uwanja wa Old Trafford jana mchana. Katika mchezo huo ambao United walipata bao lao kupitia kwa Antony Martial aliyeingia akitokea na benchi huku Stoke wakisawzisha kupitia kwa Joe Allen aliyetumia vyema makosa yaliyofanywa na david de Gea, Mourinho amekataa kuwalaumu wachezaji wake. Akihojiwa Mourinho amesema anadhani kiwango walichocheza katika mchezo huo wa jana ni bora kabisa kwa msimu huu na anadhani walistahili matokeo zaidi ya sare waliyopata.
Subscribe to:
Posts (Atom)




