Monday, November 14, 2011

STARS KATIKA KIBARUA KIZITO NA CHAD KESHO.

TIMU ya Soka ya Tanzania-Taifa Stars inatarajiwa kujitupa uwanjani kesho kupambana na timu ya Taifa ya Chad mchezo ambao utapigwa katika Uwanja Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza Dar es Salaam leo, Kocha wa Stars Jan Poulsen alitamba kuwa kikosi cha kitaibuka na ushindi katika mchezo huo ingawa amekiri kuwa haitakuwa kazi rahisi pamoja na ushindi walioupata ugenini wa bao 2-1 wiki iliyopita. Amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri nzuri kwa ajili ya mchezo huo wa kesho na kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo. Nae Kocha wa Chad Habibu Mohamed Saleh amesema kuwa kikosi chake kimekuja kwa kazi moja tu kusaka ushindi ili waweze` kusonga mbele katika hatua ya makundi. 
Akizungumzia kuhusu timu yake kupoteza mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani Saleh amesema walipoteza mchezo huo kwasababu walikuwa hawaifahamu Stars vizuri na mchezo huo umewasaidia kuwasoma vizuri na ana matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa kesho. Kama Stars wakifanikiwa kuibuka na ushindi ama sare ya aina yoyote katika mchezo huo wataingia hatua ya makundi ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Brazil 2014 wakiungana na za Morocco, Ivory Coast pamoja na Gambia katika kundi C.

Argentina Vs Bolivia 1-1 [2014 FIFA World Cup South America]

Uruguay vs Chile 4-0 Highlights 2011 Luis Suarez All Goals

MCHEZAJI MZALIWA WA NIGERIA AFIA UWANJANI UBELGIJI.

MCHEZAJI soka wa kimataifa mzaliwa wa Nigeria Bobsam Elijiko amefariki dunia baada ya kuanguka wakati wa mchezo wa ligi akiwa na timu ya Merksem Sports Club ya nchini Ubelgiji. Kwa mujibu wa taarifa za klabu hiyo Elijito alianguka katika mchezo waliokuwa wakicheza dhidi ya timu ya FC Excelsior Kaart mchezo uliocheza jana na juhudi za kuokoa maisha yake zilishindikana. Elejito ambaye alikuwa na umri wa miaka 30 katika kipindi cha karibuni aliwahi kuvitumikia vilabu vya Westerlo na Antwerp pamoja vilabu vingine mbalimbali nchini humo. Mchezo huo wa ligi ulisimamishwa baada ya kifo cha mchezaji huyo.

Saturday, November 12, 2011

ESPERANCE WATAWADHWA MABINGWA WAPYA WA AFRIKA.

TIMU ya Esperance ya Tunisia imefanikiwa kuifunga Wydad Casablanca ya Morocco kwa bao 1-0 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Rades jijini Tunis. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Casablanca timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana hivyo kupelekea Esperance kutawadhwa mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kufanikiwa kushinda mchezo huo wa pili. Bao la Esperance liliwekwa kimiani na beki wa kimataiafa kutoka Ghana Harrison Afful dakika ya 22 na kuihakikishia timu yake ubingwa wa pili wa michuano hiyo mara ya mwisho wakiwa walichukua mwaka 1994. Mbali na kikombe Esperance wamekunja kitita cha dola milioni 1.5 na ndio wataoiwakilisha Afrika katika michuano ya Klabu bingwa ya dunia itakayofanyika Japan mwakani.

VIINGILIO VYA CHAD NA STARS.

TFF imetangaza viingilio vya mchezo wa marudiano baina ya timu ya Taifa ya Tanzania-Taifa Stars na Chad mchezo unaotarajiwa kupigwa Jumanne Novemba 15 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema viingilio hivyo vitakuwa VIP A kiingilio kitakuwa shs. 20,000 VIP B shs. 10,000 VIP C 5,000 Jukwaa la Kijani na Blue mzunguko shs. 2,000 wakati Jukwaa la Rangi ya Chungwa itakuwa shs. 3,000.