Friday, July 27, 2012

FA PISSED ME OFF - CAPELLO.

Fabio Capello.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Italia, Fabio Capello amekituhumu Chama cha Soka cha Uingereza-FA kuvunja mkataba wake kwa kumvua unahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo John Terry. Capello ambaye ni raia wa Italia amesema wakati akitambulishwa kama kocha mpya wa URUSI kuwa kitendo hicho kilimuudhi sana ndio maana akaamua kuachia ngazi. Kocha huyo alichia ngazi Februari mwaka huu baada ya Terry kuvuliwa unahodha wa kikosi hicho kutokana na kukabiliwa na kesi juu ya tuhuma za ubaguzi kwa mchezaji wa Queens Park Rangers, Anton Ferdinand. Kufuatia kauli hiyo ya Capello, FA ilijibu na kusisitiza kuwa walikuwa na mamlaka ya kumvua unahodha Terry. Capello ambaye mkataba wake mpya utamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi milioni 7.8 kwa mwaka alikataa kuongelea kwa undani kuhusu Uingereza kutokana na makubaliano yake na FA.

FIFA YAMSIMAMISHA TENA BIN HAMMAM.

Mohamed Bin Hammam.
ALIYEKUWA mgombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Mohamed Bin Hammam amesimamishwa tena na shirikisho hilo ikiwa ni wiki moja tu baada ya kifungo chake cha maisha kutenguliwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo-CAS. Katika taarifa iliyotolewa na FIFA imesema kuwa Bin Hammam amefungiwa kwa siku 90 wakati Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo ikipitia na kukusanya ushahidi zaidi juu ya tuhuma za kujaribu kwanunua viongozi wan chi za Caribbean katika uchaguzi uliopita. Kamati hiyo pia itachunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha wakati Bin Hammam akiwa kiongozi wa Shirikisho la Soka barani Asia-AFC. Bin Hammam ambaye ni raia wa Qatar tayari amesimamishwa kwa muda wa siku 30 na AFC ili kupisha uchunguzi kufanyika ambapo wiki iliyopita CAS ilitengua adhabu ya kufungiwa maisha na kusema kuwa FIFA haikuwa na ushahidi wa kutosha juu ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili. Bin Hammam ambaye alikuwa mjumbe wa zamani wa kamati ya utendaji wa FIFA alichuana na Sepp Blatter katika kinyang’anyiro cha urais mwaka uliopita lakini alijitoa baada ya kutuhumiwa kuwahonga dola 40,000 kila mjumbe wa nchi za Caribbean ili wampigie kura katika uchaguzi huo.

OLIMPIKI 2012: SENEGAL YAWABANA WENYEJI.

Moussa Kanote akishangilia bao.
TIMU ya taifa ya Senegal imefanikiwa kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Uingereza katika mchezo wa ufunguzi wa kundi A wa michuano Olimpiki ambao ulifanyika katika Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester. Senegal ambao wanaingia kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo toka mwaka 1952 walisawazisha bao hilo katika dakika ya 82 kupitia kwa mchezaji wake Moussa Konate na kufuta bao lililofungwa na mkongwe Craig Bellamy mapema katika kipindi cha kwanza. Katika michezo mingine ya wanaume iliyochezwa jana Japan iliifunga Hispania bao 1-0, Honduras ilitoka sare ya bao 2-2 na Morocco, Gabon nayo ilitoa sare ya bao 1-1 wakati wawakilishi wengine wa Afrika kwenye michuano hiyo Misri walikubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Brazil. Sherehe rasmi za ufunguzi wa michuano hiyo zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Olimpiki uliopo katikati ya jiji la London baadae leo usiku.