
Tuesday, June 23, 2015
BEKI MKONGWE WA PARAGUAY AWAONYA WENZAKE KUHUSU BRAZIL.
BEKI wa timu ya taifa ya Paraguay, Paulo da Silva amewataka wachezaji wenzake kuwa makini katika mchezo wao war obo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya Brazil, akisisitiza wapinzani wao hao bado in hatari pamoja na kumkosa nahodha wao Neymar. Paraguay watakwaana na Brazil Jumamosi hii huku wakimkosa neymar ambaye amelimwa adhabu ya kutocheza mechi nne kufuatia kipigo cha bao 1-0 walichopata kutoka kwa Colombia Alhamisi iliyopita. Lakini Da Silva ambaye alikuwepo katika kikosi cha Paraguay ambacho kiliing’oa Brazil kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwaka 2011 katika michuano hiyo, bado anadhani in hatari pamoja na kumkosa nyota wake huyo. Mkongwe huyo amesema Neymar in mchezaji muhimu kea Brazil lakini pamoja na kutokuwepo timu hiyo bado inaweza kuwa na madhara kwao kwani wapo nyota wengine wanaoweza kutoa matokeo yanayohitajika. Da Silva aliendelea kudai jambo la msingi in kutobweteka na kuwa tayari kwa lolote kwenye mchezo huo kama wanataka kusonga mbele.
WAKALA AKANUSHA KUWA CECH BADO HAJAMALIZANA NA ARSENAL.
WAKALA wa golikipa Petr Cech amekanusha kuwa mteja wake huo tayari amekubali kuondoka Chelsea na kujiunga na Arsenal. Kwa kiasi kikubwa Cech anategemewa kuondoka Stamford Bridge katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi na kuhamia kea mahasimu wao Arsenal kwasababu ya kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Jose Mourinho. Hata hivyo baada ya taarifa kudai kuwa tayari Cech ameshakamilisha uhamisho huo wakala wake alizikanusha taarifa hizo kupitia mtandao wa kijamii wa twitter akidai hakuna lililoafikiwa mpaka sasa. Wakala huyo aliendelea kudai pindi kila kitu kitakapokamilika Cech mwenyewe atathibitisha hilo. Mapema jana beki wa Chelsea John Terry alidai kuwa Arsenal watanufaika sana kama wakifanikiwa kupata saini ya Cech ambaye amekaa Stamford Bridge kea miaka 11.
KOMBE LA DUNIA WANWAKE: MAREKANI, UINGEREZA ZATINGA ROBO FAINALI.
TIMU ya taifa ya Marekani imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia la wanawake kea ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Colombia. Mabao ya Alex Morgan na Carli Lloyd ambayo yalifungwa katika kipindi cha pili yalitosha kuihakikishia ushindi Marekani. Marekani washindi wa taji la michuano hiyo mwaka 1991 na 1999 ambao in moja ya timu zinazopewa nafasi ya kuibuka kidedea mwaka huu sasa watapambana China jijini Ottawa Ijumaa hii. Katika mchezo mwingine wa mtoano Uingereza nayo ilifanikiwa kutoka nyuma na kuibamiza Norway kwa mabao 2-1 na sasa watakwaana na wenyeji Canada katika kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo. Robo fainali nyingine itazikutanisha Ujerumani itakayovaana na Ufaransa wakati Australia wao wanasubiri mshindi kati ya mabingwa watetezi Japan na Uholanzi ambao wanacheza baadae leo jijini Vancouver.
HENRY AMSIFIA OZIL.
NGULI wa zamani wa soka wa kimataifa wa Ufaransa, Thierry Henry amemmwagia sifa Mesut Ozil akidai kuwa ni vigumu kumzuia wakati akiwa katika kiwango chake cha juu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Arsenal kilichonyakuwa taji la FA akiwa amefunga mabao matano na kutengeneza mengine tisa katika msimu wake wa pili akiwa na klabu hiyo. Henry ambaye anamhusudu kwa kiasi kikubwa Ozil, amesema uwepo wake katika kikosi cha Arsenal kinaifanya timu hiyo kuimarika zaidi. Henry amesema Ozil ni mchezaji mkubwa kila mtu anafahamu hilo na anafahamu kitu gani huwa anafanya katika mechi ambapo pindi anapokuwa katika ubora wake huwa ni vigumu sana kumzuia.
NEYMAR ADAD BRAZIL INAWEZA KUNYAKUWA COPA AMERICA BILA YEYE.
MSHAMBULIAJI nyota wa Brazil, Neymar anaamini kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kina wachezaji wenye ubora na uzoefu unaohitaji kea ajili ya kunyakuwa taji la michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile bila uwepo wake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 aliondoka katika kambi ya Brazil jana baada ya kulimwa adhabu ya kutocheza mechi nne kwa kosa la kumpiga kichwa Jeison Murillo wakati wa mchezo ambao Brazil ilitandikwa bao 1-0 na Colombia Alhamisi iliyopita. Lakini pamoja na kutokuwepo Neymar bado ana uhakika wachezaji wenzake waliobakia wana uwezo wa kuipeleka timu hiyo fainali na hatimaye kunyakuwa taji. Neymar mwenye umri wa miaka 23, amesema anadhani Brazil bado ina uhai bila uwepo wake kwani wachezaji wenzake wameonyesha kuwa wanaweza kushinda mechi na taji la michuano hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)