KLABU ya Watford imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco Nordin Amrabat kutoka klabu ya Malaga ya Hispania. Amrabat mwenye umri wa miaka 28 alikuwa kwa mkopo msimu uliopita katika klabu hiyo ya La Liga kabla ya kusaini mkataba wa moja kwa moja na kuitumikia mechi 15 msimu huu. Nyota huyo mzaliwa wa Uholanzi alianza kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya nchi hiyo kabla ya kuamua kuichezea Morocco. Meneja wa Watford Quique Sanchez Flores amesema Amrabat ana ubora wa wachezaji ambao wanawahitaji hivyo anadhani atawasaidia katika malengo yao.
Monday, January 18, 2016
NORWICH YAMNASA KLOSE.
KLABU ya Norwich City imefanikiwa kumsajili beki wa kimataifa wa Uswisi Timm Klose kutoka klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani kwa ada ambayo haikuwekwa wazi. Klose mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Norwich kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu akiwa amecheza mechi 39 za mashindano yote akiwa na klabu hiyo ya Bundesliga. Meneja wa Norwich, Alex Neil amesema Klose kama mchezaji amekuwa akitumia mbinu bora na pia ni mzuri wa mipira. Huo unakuwa usajili wan ne kufanywa na Norwich kipindi hiki cha Januari baada ya Matt Jarvis, Ivo Pinto na Ben Godfrey.
VIDIC AACHWA INTER.
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Serbia, Nemanja Vidic amesitishiwa mkataba wake katika klabu ya Inter Milan baada ya kushindwa kucheza mechi yeyote msimu huu. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Inter akiwa mchezaji huru akitokea Manchester United mwaka 2014 na kufanikiwa kucheza mechi 28 msimu uliopita. Vidic aliwashukuru viongozi, wachezaji na mashabiki wa Inter kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote na kuwatakia kila la kheri katika siku zijazo. Vidic amewahi kunyakuwa mataji matano ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka nane na nusu ambayo amekuwa Old Trafford.
SAKHO ANUSURIKA AJALINI.
MSHAMBULIAJI wa West Ham United, Diafra Sakho amesalimika katika ajali bila majeraha baada ya kugonga gari lake la kifahari la Lamborghini jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Senegal alithibitisha kupata ajali hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akituma ujumbe wa kushukuru kwa kutodhurika kufuatia tukio hilo. Sakho tayari alikuwa na majeruhi ya msuli ambayo yamemuweka pembeni mwa kikosi cha West Ham toka Desemba mwaka jana ambayo alipata wakati wa mchezo dhidi ya West Bromwich Albion. Sakho ameifungia West Ham mabao matano pekee msimu huu.
TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.
MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich Robert Lewandowski ameripotiwa kutofurahia kuwepo hapo baada ya nafasi ya Pep Guardiola kuchukuliwa na Carlo Ancelotti na anataka kujiunga na Paris Saint-Germain majira ya kiangazi.
Chanzo: Fechajes.net
KLABU ya Liverpool imejiunga katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez, wakati Mario Balotelli anaweza kujiunga na West Ham United. Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anadaiwa kutofurahishwa na kiwango cha Balotelli ndio maana anataka kumrejesha Hernandez Uingereza.
Chanzo: Don Balon
KLABU ya Borussia Dortmund inajipanga kumuwania kiungo wa Chelsea Ramires katika majira ya kiangazi ili kuziba nafasi ya Ilkay Gundogan ambaye anataka kwenda Juventus.
Chanzo: Fichajes.net
KLABU ya Chelsea imemuweka mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette katika mipango yao ya usajili wa majira ya kiangazi kama Eden Hazard ataondoka Stamford Bridge.
Chanzo: Fichajes.net
KLABU ya Real Madrid inajipanga kufanya usajili wake wa kwanza kipindi hiki cha Januari kwa kumtengea euro milioni 15 kiungo wa klabu ya Boca Juniors Rodrigo Betancur, ingawa bado ataendelea kuitumikia timu hiyo kwa mkopo.
Chanzo: Sport
NYOTA wa Liverpool, Jerome Sinclair anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi baada ya kushindwa kuafikiana juu ya mkataba mpya.
Chanzo: BBC

VIPIMO VYAONYESHA MESSI YUKO FITI.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameonekana kutokuwa na majeruhi yeyote baada ya kulazimika kutolewa katika muda wa mapumziko katika mchezo wa La Liga dhidi ya Athletic Bilbao. Baada ya kufunga bao la kuongoza katika ushindi wa mabao 6-0 waliopata jana katika Uwanja wa Camp Nou, nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Arda Turan baada ya kulalamika kusikia maumivu katika mguu wake wa kulia. Ilikuwa ikihofiwa kuwa mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or alikuwa amepata majeruhi ambayo yangemuweka nje kwa wiki kadhaa. Hata hivyo, baada ya kufanyiwa vipimo klabu hiyo ilithibitisha kuwa tatizo la nyota huyo mwenye umri wa miaka halikuwa kubwa kama ilivyofikiriwa. Lakini pamoja na hayo haina uhakika kama Messi atakuwepo katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Mfalme keshokutwa.
HAYATOU AJIPUNGUZIA MADARAKA CAF.
RAIS wa muda wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Issa Hayatou ameachia baadhi ya madaraka yake kama kiongozi wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kufuatia kuongezeka kwa utata katika kampeni za uchaguzi wa shirikikisho hilo. Hayatou ataachia baadhi madaraka yake hayo kwa makamu wake wawili waliopo ili waweze kusimamia shughuli za CAF katika kipindi hiki ambacho yeye atakuwa zaidi akisimamia uchaguzi wa FIFA. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mgombea urais wa FIFA Prince Ali bin al Hussein wa Jordan kulalamikia hatua ya mashirikiano iliyowekwa na CAF pamoja na Shirikisho la Soka la Asia-AFC. Hata hivyo, maofisa wa CAF walikanusha kuwa hatua hiyo ya mashirikiano haina uhusiano wowote na suala uchaguzi wa FIFA ambao unatarajiwa kufanyika Februari 26 mwaka huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)