Monday, October 31, 2011

GERRARD HATARINI KUIKOSA HISPANIA NA SWEDEN.

Steven Gerrard akishuka katika gari huku akiwa na magongo mara baada ya kutoka Hospitali.

Liverpool inasubiri kufahamu ukubwa wa jeraha la Steven Gerrard baada ya nahodha huyo kuonekana na magongo ya kutembelea huku kifundo cha mguu kikiwa kimefungwa plasta.Gerrard hakucheza siku ya Jumamosi, Liverpool ilipoilaza West Brom mabao 2-0 kutokana na kuumia kifundo cha mguu, ikiwa ni hivi karibuni tu alipona matatizo ya nyonga.Alipigwa picha akitoka hospitali akiwa na magongo na kulikuwa na taarifa alitolewa maji katika kifundo hicho cha mguu.
Kuna wasiwasi Gerrard huenda asiweze kucheza katika mechi ambayo England itapambana na Hispania pamoja na Sweden mwezi wa Novemba mwaka huu. Nahodha huyo alisafiri na kikosi cha Liverpool hadi Black Country siku ya Ijumaa, lakini baadae kifundo cha mguu wake kikaanza kuvimba siku ya Jumamosi asubuhi na hivyo kutangazwa hataweza kucheza dhidi ya West Brom.

No comments:

Post a Comment