Wednesday, November 2, 2011

SREDOJEVIC KOCHA MPYA WA AMAVUBI.



SHIRIKISHO la Soka la Rwanda-FERWAFA limemtangaza Miluntin Sredojevic kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Amavubi akichukua nafasi ya Sellas Tetteh aliyekuwa akitoka Ghana.Sredojevic ambaye alikuwa kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Sudan atakuwa akisaidiwa na wasaidizi watatu wote wakiwa raia wa Rwanda kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo.Tetteh alijiuzulu kufuatia shutuma zilizotokana na Amavubi kushindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2012 ambapo timu hiyo ilishinda mchezo mmoja kati ya mitano iliyocheza huku wa mwisho ukiwa waliocheza na Ivory Coast na kupokea kipigo cha 5-0.Kujiuzulu kwa Tetteh kulienda sambamba na kujiuzulu kwa aliyekuwa rais wa FERWAFA Jenerali Jean Bosco Kazura ambaye anafasi yake ilizibwa na Celestin Ntagugira wiki mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment