Wednesday, November 2, 2011

DROGBA KUFANYIWA UPASUAJI.

MCHEZAJI wa Chelsea Didier Drogba anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kuondoa vyuma alivyowekewa katika mkono wake wakati alipovunjika mkono mwaka jana. Chelsea inatumia nafai ya mchezaji huo kufungiwa kucheza mechi za Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo baina ya timu yake na Queens Park Ranger ili aweze kumaliza tatizo hilo. Mchezaji hakusafiri na wenzake wakati timu hiyo ilipokwenda kucheza na Genk katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini atakuwa fiti wakati timu yake itapoikabili Liverpool Novemba 20 mwaka huu.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alivunjika kiwiko chake cha mkono mwaka 2010 hali iliyotishia mchezaji huyo kucheza michuano ya Kombe la Dunia, lakini upasuaji aliofanyiwa na kuwekwa vyuma hivyo ulimwezesha kucheza michuano hiyo

No comments:

Post a Comment