SHIRIKISHO la Soka nchini Afrika Kusini -SAFA limefuta rufaa yake iliyokuwa na utata kwa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kuhusiana na utaratibu wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika.
SAFA iliwasilisha rasmi rufaa yake wiki iliyopita kwa CAF wakipinga utaratibu wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika unaotumika kuzitenganisha timu zinapokuwa zimefungana kwa kila kitu.
Shirikisho hilo pia imeomba radhi kwa nchi kutokana na timu yao ya taifa ya soka Bafana Bafana kushindwa kufuzu kucheza katika mashindano yajayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Viongozi wa SAFA ambao hivi sasa wanasakamwa sana nchini kwao baada ya timu yao kushindwa kufuzu, kimeipongeza Niger kwa kufuzu katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano.
No comments:
Post a Comment