TANZANIA imezidi kuporomoka katika viwango vya soka duniani baada ya kushuka mpaka katika nafasi ya 131 kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotolewa leo na Shirikisho la Soka la Dunia -FIFA.
Tanzania ambayo kabla ya kushuka katika nafasi hiyo ilikuwa katika nafasi ya 127, imeshuka kwa nafasi nne huku timu za Afrika zikiwakilishwa na Ivory Coast katika timu ishiriki bora baada ya wao kukamata nafasi ya 19.
Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil wamechupa mpaka nafasi ya tano huku Hispania inashika nafasi ya kwanza, Uholanzi nafasi ya pili, Ujerumani nafasi ya tatu na Uruguay nafasi ya nne zikibakia katika nafasi zake hizohizo.
Timu zingine za Afrika zinazoifuata Ivory Coast ni Misri ambayo iko nafasi ya 29, Ghana nafasi ya 33, Algeria nafasi ya 35 na Senegal nafasi ya 42.
No comments:
Post a Comment