Tuesday, November 22, 2011

BIN HAMMAM AKATA RUFANI CAS.

MOHAMED bin Hammam amekata rufani katika Mahakama ya Juu ya Kimichezo-CAS kubadilishiwa adhabu aliyopewa ya kufungiwa maisha na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia tuhuma za kununua wajumbe wa kumpigia kura wakati wa uchaguzi. Ripoti kutoka mahakama hiyo imesema katika taarifa kuwa imepokea rufani ya bin Hammam lakini bado haijapangiwa tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo. Bin Hammam atahitaji hukumu hiyo ifikapo mwezi Mei mwakani wakati Shirikisho la Soka barani Asia litakuwa bado limefungwa kisheria kuiziba nafasi yake kwa kuteua kiongozi mpya wa shirikisho hilo. FIFA ilimfungia bin Hammam mwezi Julai mwaka huu baada ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo kumkuta na hatia ya kuwanunua viongozi wa vyama vya soka vya Caribbean kumpigia kura wakati wa uchaguzi ambao alikuwa akipambana na Rais wa FIFA Sepp Blatter.

No comments:

Post a Comment