Sunday, November 6, 2011

CAPELLO KUMJUISHA TERRY KATIKA KIKOSI CHAKE.

KOCHA wa timu ya Taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema atamjumuisha John Terry katika kikosi chake kitakachopambana na Hispania na Sweden katika michezo ya kimataifa ya kirafiki leo. Kwasasa Terry yuko katika uchunguzi wa polisi pamoja na Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA kuhusu tuhuma za kumtolea maneno ya kibaguzi mchezaji wa Queens Park Rangers Anton Ferdinand. Kocha alizungumza na mchezaji Ijumaa iliyopita kuhusu suala hilo pamoja na viongozi wa juu wa FA na katika taarifa yake Capello amesema kwamba atamjumuisha mchezaji huyo katika kikosi atachokitaja hivi karibuni. Capello amesema inabidi wasubiri uchunguzi wa FA na polisi kuhusiana na suala hilo na kwamba kwasasa mchezaji huyo ni mtuhumiwa tu na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment