NEWCASTLE YAENDELEZA REKODI YAKE.
|
Ryan Taylor |
Newcastle United imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo tangu msimu msimu huu wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza ulipoanza wakati Ryan Taylor bao lake la pili lilipoizamisha kabisa Everton. Jack Rodwell alifanikiwa kufunga bao kwa kichwa baada ya kuunganisha mkwaju wa kona na kuirejeshea matumaini Everton na kulikuwa na dalili za Everton wangeweza kupatiwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili wakati Dan Gosling wa Newcastle alipounawa mpira. Lakini kikosi cha kocha Alan Pardew kilisimama imara na kujihakikishia kubakia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi. Newcastle kwa sasa haijapoteza mchezo katika ligi tangu walipopoteza mchezo kwa kufungwa mabao 3-0 mwezi wa Mei dhidi ya Liverpool msimu uliopita, lakini wanakabiliwa na mtihani mgumu katika mechi zao tatu zijazo. Robin van Persie akiwa amefunga bao la kwanza na kutengeneza mengine mawili, aliisaidia Arsenal kushinda mfululizo michezo minne iliyopita ya ligi kuu ya England. Arsenal iliizamisha West Bromwich Albion mabao 3-0. Michezo mingine iliyochezwa jana ni pamoja na Manchester United walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Sunderland, Chelsea walishinda ugenini dhidi ya Blackburn Rovers kwa bao 1-0, Liverpool walilazimishwa sare ya bila ya kufungana na Swansea City, Aston Villa walishinda mabao 3-2 dhidi ya Norwich City wakati Manchester City ambao walikuwa wageni wa Queens Park Rangers waliifunga timu hiyo mabao 3-2.
No comments:
Post a Comment