Monday, November 28, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: KILI STARS KUTUPA KARATA NYINGINE LEO.

TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjro Stars leo inatarajiwa kutupa karata yake nyingine pale itakapojitupa uwanjani kupambana na timu ya Djibouti katika mchezo wa Kombe la Challenge utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kilimanjaro ambao katika mchezo wao wa awali ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Rwanda- Amavubi inabidi kushinda`mchezo wao wa leo ili kurudisha imani kwa mashabiki na kuweka matumaini hai ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Mabingwa hao mara tatu wa michuano hiyo leo huenda wakamkosa mshambuliaji wao hatari Mbwana Samata anaesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu baada ya kuumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda. Katika mchezo mwingine utakaochezwa mapema mchana huu timu ya Rwanda itapambana na Zimbabwe huku timu zote zikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda michezo yao ya kwanza.

No comments:

Post a Comment