Wednesday, November 30, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: ZANZIBAR HEROES KUTUPA KARATA YAO YA MWISHO.

TIMU ya taifa ya Zanzibar-Zanzibar Heroes leo inatarajia kutupa karata yake ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji itavaana na Somalia katika mchezo wa kundi B utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Zanzibar ambayo katika mchezo wao wa kwanza ilikubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Uganda na kutoa sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa pili dhidi Burundi itakuwa ikiomba Uganda waifunge Burundi ili waweze kupata nafasi ya kusonga mbele. Timu hiyo ambayo mbali na kuomba ushindi kwa timu ya Uganda lakini pia wao itabidi wawafunge Somalia mabao yasiyopungua manne. Matokeo yakiwa hivyo Zanzibar itakuwa imefungana pointi na Burundi wote wakiwa na alama nne hivyo Zanzibar kusonga mbele kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga na kuiacha Burundi ikirejea nyumbani.

No comments:

Post a Comment