Thursday, December 1, 2011

RATIBA YA EURO 2012 KUPANGWA KESHO.

RATIBA ya michuano ya Kombe la Ulaya 2012 inatarajiwa kupangwa kesho jijini Kiev, Ukraine huku kila timu ikiomba iepuke kupangwa kundi moja na Hispania. Timu hiyo ambayo ndio inapigiwa chapuo kuwa timu ya kwanza kushinda mataji matatu makubwa itakuwa na Uholanzi pamoja na Poland na Ukraine kuwa timu za juu katika mchakato huo. Timu zingine 12 zimegawanywa katika makundi mengine matatu wadau wengi wakidai itakuwa ratiba ngumu haswa kama mkipangwa kundi moja na timu kama Hispania, Ujerumani na Uholanzi. Timu nyingi zitapenda kupangwa katika kundi A ambapo iatkuwepo Poland na Kundi D ambapo itakuwemo Ukraine kwa kuwa sio timu zinazotisha sana.

No comments:

Post a Comment