Thursday, December 1, 2011

SUPER COACH COURBIS KUINOA NIGER.

SHIRIKISHO la Soka nchini Niger limemtaja kocha wa zamani wa timu ya Marseille Roland Courbis kuwa mshauri wa timu hiyo katika kipindi cha michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka kesho. Kocha huyo raia wa Ufaransa atakuwa akimsaidia kocha mkuu wa timu hiyo Harouna Douala ambaye ameisaidia timu hiyo kufuzu kwa mara kwanza kucheza michuano hiyo. Akizungumzia uteuzi huo rais wa NFF amesema kuwa Roland atakuwa kama mshauri pamoja na kubadilishana uzoefu wake na Harouna katika kipindi cha mashindano hayo kwasasa Roland tayari amekwisha jiunga na kikosi hicho kilichopo Dubai kwa mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Botswana.

No comments:

Post a Comment