Thursday, December 1, 2011
MICHUANO YA KUFUZU OLIMPIKI YAPAMBA MOTO.
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 ya Misri jana imeshindwa kupata ushindi waliohitaji ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Olimpiki baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ivory Coast. Kwa upande wa mchezo wa kundi B Afrika Kusini na Gabon zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na kwa matokeo hayo timu zitazoingia hatua ya nusu fainali zitajulikana Jumamosi katika michezo yao ya mwisho. Katika michezo itakayochezwa Jumamosi Ivory Coast itapambana na Gabon wakati Afrika Kusini itajaribu kutupa karata yake ya mwisho kwa Misri. Katika michuano ambayo imekuwa na msisimko mkubwa safari hii timu zote nane zina nafasi ya kucheza michuano ya Olimpiki kama wakishinda michezo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment