SLFA HATARINI KUFUNGIWA.
Shirikisho la Soka la Sierra Leone-SLFA linaweza kufungiwa na Shirikisho la Soka duniani-FIFA kufuatia serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala mpira. Hayo yamekuja kufuatia Ligi Kuu ya nchi hiyo kusogezwa mbele na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Paul Kamara kufuatia mkutano ulioandaliwa na serikali kufuatia mgogoro unaoikabili ligi hiyo. Shirikisho la soka nchi liliomba serikali kutoingilia masuala yao ya mpira huko mbeleni lakini wizara ikasisitiza kuwa kusogezwa mbele kwa ligi hiyo ni makubaliano ya klabu husika.
No comments:
Post a Comment