
Friday, December 2, 2011
O'NEILL AKUBALI KUINOA SUNDERLAND.
Martin O’Neill amekubali kuchukua mikoba ya aliyekuwa meneja wa Sunderland Steve Bruce ambaye alitimuliwa na klabu hiyo siku zilizopita baada ya timu hiyo kusuasua katika Ligi Kuu ya Uingereza. O’Neill ambaye kwa mara ya mwisho alikuwa anainoa klabu ya Aston Villa amekuwa akitajwa mara kwa mara kuzinoa klabu mbalimbali za ligi kuu katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Kocha huyo mwenye miaka 59 ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Nottingham Forest alianza kazi ya ukocha katika klabu ya Wycombe kabla kuhamia Leicester City na Celtic ambazo alizinoa kwa mafanikio. Alichukua kibarua cha kuinoa klabu ya Aston Villa mwaka 2006 na kuisaidia klabu kumaliza ikiwa katika nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu katika misimu mitatu mfululizo na kuingoza timu katika fainali kombe la ligi kabla ya kuachia ngazi kibarua chake hicho mapema kabla ya kuanza kwa msimu wa 2010-2011.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment