Friday, December 2, 2011
MARADONA AMBWATUKIA PELE.
MWANASOKA nguli wa zamani kutoka Argentina ambaye kwasasa ni kocha wa timu ya Al Wasl Diego Maradona amemtuhumu mchezaji mwenzie nguli wa zamani kuwa alikunywa dawa ambazo hazikutakiwa. Kauli ya kocha huyo imekuja wakati akihojiwa jana kufuatia Pele kudai kuwa mshambuliaji wa timu ya Santos Neymar ni mchezaji bora zaidi ya mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. Maradona alimshambulia Pele kwa kumwambia kuwa alikunywa vidonge ambavyo havikutakiwa kabla ya kuongea aliyoyaongea wakati akihojiwa na waandishi wa habari. Maradona pia amesema kuwa mchezaji huyo nguli wa zamani mwenye umri wa miaka 71 alikuwa amechanganyikiwa na alikuwa hajui asemalo na akampa ushauri mara nyingine kabla ya kuongea anatakiwa kunywa vidonge stahili au abadilishe daktari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment