Tuesday, November 22, 2011

ETO'O, ENOH WAITWA KAMATI YA NIDHAMU.

KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini Cameroon-Fecafoot imewaita wachezaji Samuel Eto’o na Eyong Enoh kwasababu ya kuchochea mgomo wiki iliyopita. Sakati limeibika baada ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Cameroon kugoma kwenda Algeria kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu hiyo kutokana na kutolipwa marupurupu yao katika michezo miwili iliyopita waliyocheza na Morocco pamoja na Sudan. Wachezaji hao walitarajiwa kufikishwa mbele ya kamati hiyo jana, lakini waliomba shauri hilo liahirishwe mpaka hapo maafisa wa Fecafoot nao watakapoitwa na kamati hiyo. Mbali na kina Eto’o pia Benoit Assou-Ekotto ambaye ni beki wa Tottenham Hotspurs nae ameitwa na kamati hiyo kwa kosa la kutojiunga na kikosi hicho katika mchezo dhidi ya Morocco pamoja na mechi waliyosusia ya Algeria.

No comments:

Post a Comment