Tuesday, November 22, 2011

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BAYERN, UNITED, INTER KIBARUANI LEO.

MABINGWA wa zamani wa Ulaya timu za Bayern Munich, Manchester United na Inter Milan zitajitupa uwanjani kutafuta nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika michezo yao itakayochezwa Jumanne hii. Bayern wenyewe watahitaji suluhu dhidi ya timu ya Villarreal watakayocheza nayo ambayo imepoteza michezo yake yote katika kundi A na kuingia hatua hiyo ya mtoano wakati United itahitaji ushindi dhidi ya Benfica ili kujihakikishia nafasi hiyo. Inter nao watahitaji suluhu katika mchezo wao wa leo dhidi ya Trabzonspor ili kujihakikishia nafasi ya kujiunga na majirani zao AC Milan ambao tayari imeshasonga mbele katika hatua ya makundi wakati mabingwa mara tisa wa michuano hiyo Real Madrid itabidi ishinde mchezo wao wa kundi D dhidi ya Dinamo Zagreb ili kuhakikisha wanamaliza wakiwa wanaongoza kundi hilo. Michezo mingine itayochezwa leo ni pamoja na Manchester City ambao itahitaji ushindi dhidi ya Napoli ili kusonga mbele, SCKA Moscow wataikaribisha Lille wakati Otelul Galati itacheza na Basle.

No comments:

Post a Comment