Sunday, November 27, 2011

MANCINI AWACHARUKIA WACHEZAJI WA LIVERPOOL.

MENEJA wa Manchester City Roberto Mancini amedai kuwa wachezaji wa Liverpool wanapaswa walaumiwe kufuatia kutolewa kwa mshambuliaji wake Mario Balotelli wakati timu hizo zilipotoka sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Anfield. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Italia alitolewa nje baada ya kupata kadi mbili za njano ikiwa ni dakika 18 tu toka aingie akitokea benchi. Mancini amesema hakubaliani na kadi ya pili aliyopewa mchezaji huyo kwani mwamuzi hakutaka kumpa kadi hiyo hadi pale wachezaji wa Liverpool walivyomzonga mwamuzi huyo kumlalamikia. Balotelli alipewa kadi ya kwanza ya njano kwa kosa la kumvuta mchezaji wa Liverpool Glen Johnson wakati kadi ya pili ya njano alipewa kufuatiwa kumshika Martin Skrtel kwa mikono.

No comments:

Post a Comment