Friday, November 11, 2011

ROAD TO BRAZIL 2014: KENYA, NAMIBIA, CONGO ZAANZA KWA KISHINDO.

TIMU za Namibia, Kenya na Jamhuri ya Congo zimepata ushindi mnono ugenini wakati timu zilizo chini katika viwango vya Shirikisho Soka Duniani-FIFA zilipokuwa zikitafuta nafasi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 jana. Namibia waliichabanga bila ya huruma kwa mabao 4-0 timu ya Djibouti na Kenya ambao walikuwa wageni wa Seychelles walipata ushindi wa mabao 3-0 wakati Jamhuri ya Congo wenyewe waliipiga bila ya huruma Sao Tome de Principe kwa mabao 5-0. Togo ambao wameshawahi kushiriki michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Ujerumani mwaka 2006 walijikuta waking’ang’aniwa na ugenini na Guinea Bissau. Michezo mingine iliyochezwa jana ni pamoja na Comoros walipata kipigo nyumbani cha bao 1-0 kutoka kwa Msumbiji, Eritrea walitoshana nguvu na Rwanda kwa kwenda sare ya bao 1-1, Equatorial Guinea iliifunga Madagascar mabao 2-0, Swaziland walishindwa kutumia uwanja wao nyumbani baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wakati Lesotho waliitambia Burundi kwa kuifunga bao 1-0. Leo kutachezwa mchezo mmoja ambapo Somalia itapambana na Ethiopia mchezo ambao utachezwa jijini Mogadishu kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Somalia.

No comments:

Post a Comment