Wednesday, November 2, 2011

TUSKER CHALLENGE CUP: SBL YAMWAGA MAMILIONI.

Mkurugenzi wa SBL Richard Welles akimkabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shs. Milioni 823 Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye huku Mwenyekiti wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Leodgar Tenga na Katika Mkuu wa TFF Angetile Osiah wakishuhudia tukio hilo.
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti-SBL kupitia bia yake ya Tusker imemwaga kitita cha shilingi milioni 823 kwa ajili ya udhamini wa mashindano ya CECAFA Tusker Challenge Cup itakayofanyika mwaka huu.Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya hundi hiyo, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa SBL Richard Wells amesema fedha walizotoa zitagharamia mahitaji kama vile tiketi za ndege msafara wote wa CECAFA pamoja na viongozi wa shirikisho hilo, malazi, usafiri, watoa huduma, fedha za washindi, malipo ya CECAFA ndani na nje ya nchi, kodi ya uwanja, ulinzi na sehemu ya mazoezi kwa wachezaji.
Tenga akifafanua jambo huku Jaji Mark Bomani (kushoto) ambaye ndio Mwenyekiti wa Bodi ya SBL akimsikiliza.


Welles pia amesema fedha hizo zitatumika kuratibu waandishi wa habari na mahitaji mengie ya utawala ambapo michuano hiyo inatarajiwa kutimua vumbi kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 10 mwaka huu.Amesema michuano hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa kukuza vipaji na kuendeleza mchezo soka hapa nchini pamoja na nchi zilizopo mashariki mwa Afrika ambapo timu zitakazoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Djibout, Somalia, Ethiopia, Sudan, Zanzibar, Eritrea na wenyeji Tanzania.

No comments:

Post a Comment