Wednesday, November 2, 2011

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA, AC MILAN ZASONGA MBELE

TIMU za Barcelona na AC Milan zimekuwa za kwanza kukata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano ya timu 16 bora katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya. Katika mchezo wa Barcelona mshambuliaji wake machachari Lionel Messi alifunga Hat-Trick wakati timu yake hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Plzen wakati AC Milan wao walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bate Borisov. Arsenal na Chelsea zilishindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano baada ya kulazimishwa sare ambapo Arsenal waliokuwa wenyeji wa Marseille walishindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kukubali suluhu ya bila ya kufungana. Chelsea ndio walioanza kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Ramirez kabla David Luiz kukosa penati na kuipa nafasi Genk kusawazisha bao muda mchache kabla ya mapumziko hivyo kupelekea mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Mechi nyingine zilizochezwa jana na matokeo ni pamoja na Apoel Nicosia 2-1 FC Porto, Borussia Dortmund 1-0 Olympiokos, Valencia 3-1 Bayer Liverkusen na Zenit St Petersburg 1-0 Shakhtar Donetsk.

No comments:

Post a Comment