Saturday, January 7, 2012
ADHABU YA KINA ETO'O YABADILISHWA.
KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Cameroon-Fecafoot limebadilisha adhabu ya kufungiwa kwa nahodha wake Samuel Eto’o mechi 15 na sasa atatumikia miezi nane katika adhabu hiyo. Maamuzi hayo yalifikiwa na kikao cha mwisho kilichokaa kamati hiyo jana usiku katika jiji la Yaounde nchini ambapo pia adhabu za wachezaji wengine wa timu hiyo pia zilibadilishwa. Eto’o alikumbwa na adhabu hiyo baada ya kuwaongoza wachezaji wenzake wa timu ya ya taifa ya nchi hiyo kugoma wakidai posho zao. Wachezaji wengine waliobadilishiwa adhabu ni pamoja na nahodha msaidizi wa timu hiyo Eyong Enoh ambaye adhabu yake ya mechi ilibadilishwa kuwa miezi miwili wakati Assou Ekotto ambaye yeye ametozwa faini ya dola 5,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment